UJENZI WA DARAJA LA LIBANGO WILAYANI NAMTUMBO WAKAMILIKA,
Na Muhidin Amri, Namtumbo
WANANCHI wa kijiji cha Libango katika Halmashauri ya wilaya Namtumbo mkoani Ruvuma,wameishukuru wakala wa barabara za vijijini na mijini(Tarura),kujenga daraja la kudumu linalounganisha kijiji hicho na mji wa Namtumbo.
Wamesema,daraja hilo limemaliza mateso waliyokuwa nayo kwa muda mrefu ya kuvuka kwenye maji baada ya daraja la zamani lililojengwa kwa vyuma na serikali ya awamu ya pili kusombwa mwaka mmoja uliopita.
Imani Mtotomwema ameeleza kuwa,kukamilika kwa ujenzi wa daraja hilo ni ukombozi mkubwa kwa wananchi wa kijiji cha Libango na vijiji vingine vya kata ya Namtumbo mjini ambao watalitumia kwenye shughuli zao za uzalishaji mali.
“tunaishukuru sana serikali ya Rais Samia kwa ujenzi wa daraja hili maana ndiyo kilikuwa kilio chetu cha muda mrefu kwa sababu wananchi wote wa Libango mahitaji yetu yote tunapata Namtumbo mjini”alisema.
Aidha alisema kuwa, kukosekana kwa daraja katika eneo hilo ilipelekea maisha yao kuwa magumu kwani hawakuweza kuvuka mto Luegu wenye maji mengi kwenda maeneo mengine kupata mahitaji na huduma za kijamii.
Alisema wananchi wengi wa Libango ni wakulima,lakini walishindwa kusafirisha mazao yao kwenda sokoni,hali iliyosababisha umaskini na gharama za maisha kuwa juu.
Adinan Sadik mkazi wa Namtumbo alisema,wananchi wa kijiji cha Libango walishindwa kupata huduma za kijamii kutokana na kukosekana kwa mawasiliano baada ya daraja hilo kusombwa na maji ambapo baadhi ya akina mama wajawazito kushindwa kufika katika vituo vya kutolea huduma kwa wakati.
Mfaume Katondo dereva wa bajaji alisema,daraja hilo limerahisisha kuzifikia huduma mbalimbali za kijamii na kufungua fursa za kiuchumi kwa wakulima ambao watapeleka mazao moja kwa moja sokoni kuuza mazao yao ,badala ya wanunuzi kununua mazao shambani kwa bei ndogo.
“tumefarijika sana kuona ujenzi wa daraja hili umekamilika,daraja hili linakwenda kutatua matatizo yote ya hapo awali ambayo yalikuwa yakitukabili,sasa Libango inakwenda kufunguka”alisema Katondo.
Kwa upande wake Meneja wa Tarura wilaya ya Namtumbo Fabian Lugalaba alisema,ujenzi wa daraja la Libango umefanyika kwa awamu mbili ambapo katika awamu ya kwanza ilikuwa ni usanifu na awamu ya pili ni ujenzi wa daraja lenyewe lenye upana wa mita 30.
Alieleza, katika awamu ya tatu itahusisha ujenzi wa box kalavati ndogo ili kuruhusu maji kupita upande mwingine,kujaza udongo na kufanya matengenezo ya barabara ya Namtumbo –Libango yenye urefu wa kilomita 14 kwa kiwango cha changarawe.
Lugalaba alitaja gharama za ujenzi wa mradi huo ni shilingi bilioni 1,390 kati ya hizo shilingi milioni 890 ni za ujenzi wa daraja na shilingi milioni 500 zitatumika kufanya matengenezo ya barabara.

Kwa mujibu wa Lugalaba,wakala wa barabara Tanzania(Tarura) wilaya ya Namtumbo,unaendelea na mpango wake wa kufungua barabara ili kufika kusiko fikika katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo ili kuboresha na kuharakisha upatikanaji wa huduma za kiuchumi na kijamii kwa wananchi.Muonekano wa sehemu ya juu ya daraja la Libango wilayani Namtumbo.Daraja la Libango linalounganisha kijiji cha Libango na mji wa Namtumbo kama linavyoonekana baada ya ujenzi wake kukamilika na limeanza kutumika kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo.Magari yakianza kupita katika daraja la Libango wilayani Namtumbo baada ya wakala wa barabara za vijijini na mmijini Tanzania(TARURA)kukamilisha kazi ya ujenzi wake.
Post a Comment