Header Ads

test
Na Jane Edward, Arusha

Kamati ya bunge ya Ardhi na maliasili imeipongeza shirika la nyumba la Taifa kwa ujenzi wa soko la madini ya Tanzanite linalo jengwa Mkoani Simanjiro mji mdogo wa Mererani.

Akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea jengo hilo linaloendelea na ujenzi Mwenyekiti wa kamati ya Bunge Ardhi na Maliasili Timoth Mzava amesema wamefurahishwa na hatua iliyochukuliwa na serikali ya awamu ya sita katika mradi wa ujenzi wa soko la madini ya Tanzanite lenye ghorofa tano .

Amesema kwa kutambua umuhimu wa jengo hilo shirika la nyumba liongeze kasi ya ujenzi wa jengo hilo ili kuweza kuwanufaisha wakazi wa Simanjiro katika ajira pamoja na mambo mengine.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu shirika la nyumba la Taifa (NHC)Hamad Abdallah amesema ugeni wa kamati ya bunge ya Ardhi na Maliasili katika kukagua taasisi zilizo chini ya Maliasili na Ardhi ambapo mradi huo ambao wamepewa na halmashauri ya Simanjiro ili kujenga kwa lengo la kutumika kama soko la madini ya Tanzanite.

"Mradi huu tunataraji utakamilika mwezi wa sita kwa kuwa tayari vijana wako kazini na ili kwenda na kasi inayotakiwa jengo hili litajengwa usiku na mchana"Alisema Hamad

Ameongeza kuwa jengo hilo litakuwa la mfano na pia itakuwa imetengeneza muonekano Mzuri wa mji wa Simanjiro kwa kuzingatia madini yalikuwa yakiuzwa Mkoa wa Arusha

Akizungumzia changamoto Mkurugenzi huyo amesema gharama za vifaa vya ujenzi imekuwa changamoto kupata malighafi nje ya Tanzania ili kutengeneza nondo za kujengea jengo hilo kwakuwa haiwezi kutengenezwa na vyuma chakavu.

Aidha amesema gharama za ujenzi ni takribani Bilioni 5 ili kukamilisha ujenzi huo wa awali ili kuanza kutumika jengo hilo rasmi.

Naibu waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Joseph Mizengo Pinda ameishukuru kamati ya bunge kwa kutembelea moja ya miradi ya kimkakati wanayoisimamia kama wizara na kuwaahidi kukamilika kwa jengo hilo kwa wakati.

"Serikali ya Rais Samia imesikia kilio cha wananchi wa Mkoa huu na kuamua kuleta soko la Tanzanite hapa ili wananchi waweze kunufaika na madini hayo ambayo yanapatikana Tanzania pekee"Alisema Pinda.







No comments