Header Ads

test

PONGEZI MIAKA MIWILI YA RAIS DKT SAMIA SULUHU HASSAN KUTOKA LUDEWA.

 




-WILAYA YA LUDEWA, ILIYOPO MKOANI NJOMBE- TUNASEMA ASANTE SANA

Kwa hakika miaka yako miwili imekuwa ya Neema na baraka tele kwetu wana-Ludewa, umekuwa ukiitazama Wilaya yetu kwa jicho la upekee sana.


Tumeshuhudia miradi mikubwa na ya fedha nyingi ikija ndani ya Wilaya yetu kama,

1. Tumepata Sh. Bilioni 2.6 kwaajili ya ufunguzi wa barabara za Mwambao.

2. Tumepata Sh. 2.8 Bilioni kwaajili ya ujenzi wa Ofisi za Halmashauri ya wilaya ya Ludewa, Milioni 500 za ujenzi wa Ikulu, na Milioni 150 za ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi ( DED )

3. Tumepata Sh. 5.4 Bilioni kwaajili ya ujenzi wa Chuo cha VETA Shaurimoyo.

4. Tumepata Sh. 179 Bilioni kwaajili ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha zege Lusitu - Mawengi.

5. Tumepata kiasi cha Sh. 5.4 Bilioni kwaajili ya ujenzi wa barabra eneo la Mlima Kimelembe ambao utaongeza usalama wa safari wilayani mwetu

6. Tumepata Milioni 900 kwaajili ya ukarabati wa Hospitali ya Wilaya, Milioni 250 kwaajili ya ujenzi wa jengo la ICU Hospitali ya Wilaya, Milioni 500 kukamilisha kituo cha Afya Mundindi, na ujenzi wa zahanati 16 ambapo nne zimesha kamilika na zinatoa huduma ( Mholo, Nsisi, Mdilidili na Lifua ),huku 12 zikiendelea na ujenzi ( Mkiu, Kimelembe, Ndowa, Chimbo, Liunji, Lihagule na Mbongo, Sagalu, Ludewa kijijini, Kimata, Nsele na Mbugani).

7. Tumepata fedha za miradi ya maji Kata ya Mawengi wame pewa Bilioni 2, Mavala Bilioni 1, Mavanga Bilioni 1.5, Luvuyo Bilioni 1.5, Madope Milioni 508, Lifua na Manda Milioni 600 na kata ya Ludewa Bilioni 7.

8. Tumepata minara ya simu mipya 7 ambayo inatoa huduma na mwaka huu tunarajaia kuanza ujenzi wa minara mingine sita.

9. Ujenzi wa daraja mto ruhuhu, ambalo limeokoa wananchi wengi wa kata ya Ruhuhu kuliwa na Mamba

10. Ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Lubonde ambayo kiasi cha Sh. 470 Milioni kutoka Serikali kuu na Milioni 55.5 kutoka mapato ya ndani yametumika na imeanza kutoa huduma, ujenzi wa maabara mpya 12, ujenzi wa vyumba 41 vya madarasa S/M na Vyumba 81 S/Sekondari

11. Tumepata zaidi ya Bilioni 10.3 kwaajili ya ujenzi wa barabra vijijini kupitia Tarura.


NENO LETU NI ASANTE MHESHIMIWA RAIS DKT SAMIA SULUHU HASSAN

Kwa hatua hizi na nyingine nyingi za kimaendeleo katika Wilaya ya Ludewa


#LudewaYetu

Taarifa hii ni Kwa Hisani ya Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mhe.Victoria Mwanziva



No comments