Na Janeth Raphael - MichuziTv Dodoma
Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) limewatunuku Wakunga na Wauguzi 1949 vyeti vya Usajili, Uorosheshwaji na Leseni waliofuzi Shahada ya kwanza, Stashahada na Astashahada ya Uuguzi na Ukunga.
Baraza la Uuguzi na Ukunga ni Mamlaka ya kisheria inayosimamia Taaluma ya Uuguzi na Ukunga Tanzania chini ya Sheria ya mwaka 2010 ( the Nursing and Midwife Ac, 2010)
Akizungumza katika Mahafali hayo yaliyofanyika jijini Dodoma katika Ukumbi wa Mabeyo Mwenyekiti wa Baraza hilo Profesa Lilian Mselle amesema wahitimu hao wamepata vyeti pamoja na leseni wataongeza nguvu kazi katika sekta ya afya na orodha ya wauguzi na wakunga hapa Nchini.
Profesa Lilian amewaambia wahitimu hao kuwa huduma nzuri ni zile zinazozingatia weledi na umahiri, maadili na uaminifu pia kuwajali wagonjwa

" Zingatieni miiko, taratibu na miongozo inayohusu taaluma zenu kama mlivyofundishwa." Amesema Profesa Lilian.
Profesa Lilian Mselle amesema kuna baadhi ya wauguzi na wakunga hawatimizi majukumu yao ipasavyo hivyo kama Baraza wataendelea kuchukua hatua za kisheria kwa wale watakaokengeuka maadili ya taaluma zao.
Hata hivyo Profesa Lilian amewataka wahitimu hao kujielimisha katika maeneo mbalimbali ya kitaalima na kisaidia kuelimisha wengine wenye mapungufu kwani wakiwa na lengo moja watatoa huduma zilizo sahihi, bora na salama.
Naye Mwenyekiti Baraza la Uuguzi na Ukunga upande wa Zanzibar Amina Abdlikadir Ali amesema ni wakati sasa wa kwenda kutekeleza yale wahitimu hao waliyojifunza na kuwakumbusha mambo matatu wanayotakiwa yawepo midomoni mwao kila mara...

" Tafadhali, ahsante na samahan na pia kuhudumia vyema wagonjw." amesema
Amewaeleza wahitimu hao kuwa wakumbuke huduma hata wawe wamechoka vipi watambue kuwa Mungu amewaleta kuwa Wauguzi na Wakunga hivyo ni jukumu lao kuwahudumia wale wenye uhitaji.
Awali akimkaribisha mgenie rasmi Msajili Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) Agness Mtawa amesema mahafali hayo ni ya saba tangu kuanzishwa Kwa baraza hilo mwaka 1953.
Aidha Msajili huyo amesema pamoja na mafanikio hayo bado kuna changamoto ambapo bado kuna shida ya uvunjifu wa maadili Wakunga na Wauguzi kutohuisha Leseni zao kwa muda na bila sababu za msingi na pia kuna wajanja wanaoingilia taaluma bila kuwa nae elimu.

Agness amesema hata hivyoe wanaendelea kutoa elimu ya maadili ya Mafunzo na usimamizi, kuhamisha wana taaluma hao kuhakikisha wakati wote wanatembea wakiwa na Leseni zao zilizo hai.
Mwisho wahitimu katika mahafali hayo Emmanuel Mkinga pamoja na Agness Mdemu kwa nyakati tofauti wametoa ushauri kwa viongozi wa Baraza hilo kuhakikisha wanatenda haki na kutoa wauguzi ambao wana vigezo ili kuongeza tija kwa wafanyakazi na fani ya wauguzi na wakunga iweze kuendelea, na jamii itegemee kupata huduma bora kutoka kwa Wauguzi na Wakunga kwa sababu tumejifunza mengi na waondoe hofu na dhana potofu.
Sherehe hizo za Mahafali ya saba yameambatana na maadhimisho ya miaka 70 ya baraza hilo anbapo kauli mbiu ya mwaka huuu ni...
BIMA YA AFYA KWA WOTE. " Muuguzi na Mkunga ni tarajio la huduma bora kwa jamii'

Mwenyekiti Baraza la Uuguzi na Ukunga upande wa Zanzibar Amina Abdlikadir Ali akizungumza katika sherehe ya mahafali ya saba ya baraza hilo yaliyofanyika jijini Dodoma katika Ukumbi wa Mabeyo
Mwenyekiti wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) Profesa Lilian Mselle akizungumza katika sherehe ya mahafali ya saba za baraza hilo yaliyofanyika jijini Dodoma katika Ukumbi wa Mabeyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Baraza la Uuguzi na Ukunga wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi waliopo meza kuu.
Msajili Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) Agness Mtawa akizungumza katika sherehe ya mahafali ya saba ya baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania yaliyofanyika jijini Dodoma katika Ukumbi wa Mabeyo.

Post a Comment