SEKO SHAMTE ATOA SHAVU KIWANDA CHA BONGOMUVI KIMATAIFA
Na.Khadija Seif, Michuziblog
NAIBU Waziri wa ,Utamaduni na Sanaa na michezo amewataka watayarishaji wa kazi za Filamu nchini kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha sanaa inafika mbali zaidi na kutafuta masoko ya kimataifa kupitia kazi zao.
Akizungumza na Waandishi Wahabari Jijini Dar es salaam Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Khamis Mwinjuma amesema Serikali inafanya kila jitihada kuhakikisha inawapa nguvu Wasanii ili kutengeneza kazi zenye ubora wa Kimataifa na ndio sababu kuwepo kwa Mikopo bila riba.
Hata hivyo Mwinyijuma amempongeza Mtayarishaji wa filamu nchini Seko shamte kwa kuwapa kipaumbele wasanii na watayarishaji wa kazi za Filamu kushirikiana katika mradi huo wa Kimataifa kuhakikisha wanatengeneza filamu lenye lengo la kutoa Elimu kuhusu ugonjwa wa virusi vya Ukimwi na namna ya kukabiliana nao.

"Nikiona tamthilia ya Seko Shamte "Binti" kwenye Netflix Huwa nawaza kuwa Seko amepiga pesa nyingi hivyo mradi huu uliofadhiliwa na (PEPFAR)wenye pesa nyingi billion 6.6 Kuna sehemu ipo wazi kuwa wasanii na Watayarishaji na Wasanii wamenufaika kupitia mradi huo kwa kiasi fulani.''
Pia ametoa rai kwa wasanii na watayarishaji kutengeneza kazi zenye ubora na viwango ili kufikia soko la Kimataifa kutokana na sekta ya Sanaa kukuwa siku hadi siku na kuwa na wadau wengi kwa sasa.
Kwa upande wake Muaandaaji wa Filamu hizo Seko Shamte amesema lengo la kutengeneza filamu hizo ni kutoa Elimu kwa jamii ya Kitanzania hivyo filamu hizo zitaonyeshwa clouds tv kuanzia saa 3 usiku kuanzia machi 23,2023 .
"Niliamua kuwapa nafasi watayarishaji, wasanii na waandaaji wa Kazi za Filamu kwa upande wa watanzania zaidi kwani kuna vipaji vingi."

Hata hivyo Shamte amesema kupitia filamu hizo wataendelea kutoa elimu kwa jamii ili kufikia lengo la kupunguza maambukizi ya virusi vya Ukimwi nchini kama Mradi wenyewe unavotoa muongozo wake.Picha ya pamoja katia ya Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma, Katibu Mtendaji wa bodi ya Filamu Dkt.Kiagho Kilonzo, Seko Shamte pamoja na Wasanii mbalimbali walioshiriki Filamu 3 sweta,jasiri pamoja na Nia zilizotayarishwa na Seko Shamte kwa ufadhili wa Mradi wa Pepfar kutoka Marekani.Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma akizungumza na Wanahabari Leo Machi 15,2023 mara baada ya kuzindua rasmi Filamu 3 Sweta,Jasiri pamoja na Nia zilizoandaliwa na Mtayarishaji Seko Shamte zilizofadhiliwa na Mradi kutoka Marekani wenye lengo la kupambana na maambukizi ya virusi vya Ukimwi na kutoa elimu kushoto kwa Naibu Waziri ,Katibu Mtendaji wa bodi ya Filamu nchini Dkt.Kiagho Kilonzo pamoja na kulia kwake ni mtayarishaji wa filament hizo Seko Shamte.
Post a Comment