Header Ads

test

PSSSF YAPOKEA UGENI KUTOKA SERIKALI NA BUNGE LA UGANDA

 


·       Kiongozi wa Msafara Bi Catherine Musingwilire asifia juhudi zinazofanywa na SSH na kusifia Tanzania kuwa ni sawa na nyumbani kwake

·      DG Kashimba aahidi kuendeleza ushirikiano na amefurahishwa na kufarijika na ujio huo 

UJUMBE kutoka Serikali na Bunge la Jamhuri ya Uganda umefanya ziara ya mafunzo PSSSF kwa ajili ya kujifunza namna ya uendeshaji wa huduma za hifadhi ya jamii kwa waajiriwa wa Serikali, kufuatia maboresho ya kisera ya kuanzisha Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma unaoanzisha rasmi utaratibu wa kuchangia kupitia muswada wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma wa mwaka 2023; uliowasilishwa Bungeni na Serikali ya Uganda mnamo tarehe 14 Machi 2023.

Akiukaribisha ugeni huo Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF CPA. Hosea Kashimba alisema amefarijika sana kwa heshima hiyo na ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano na ushauri kila mara itakapohitajika.    Aidha mkuu wa msafara huo Katibu Mkuu wa Wizara inayoshughulikia Utumishi wa Umma Bi. Catherine Musingwiire ameushukuru uongozi wa PSSSF kwa kuwapatia elimu na uzoefu wa kina wa namna bora za uendeshaji wa Mfuko kupitia mifumo ya ukusanyaji michango, uwekaji wa kumbukumbu za wanachama, huduma za kidijitali za wanachama pamoja na upande wa uwekezaji ili kuhakikisha uendelevu wa Mfuko. 

Mada mbalimbali ziliwasilishwa na watendaji wa Mfuko wakiwemo Mkurugenzi wa Uendeshaji Mbaruku Magawa, Mkurugenzi wa Hadhari na Majanga Ansgar Mushi,  Mkurugenzi wa Huduma za Sheria Vupe Ligate, Afisa Mkuu wa Huduma za Sheria Valentino Daudi na Kaimu Mkurugenzi wa TEHAMA Mariam Saleh.  Wawasilishaji hawa walisisitiza umuhimu wa kuweka mazingira wezeshi kuendana na mabadiliko, ushirikishwaji wa utatu (Serikali, Vyama vya Wafanyakazi na Waajiri), utayari wa kisiasa, huduma bora na matumizi ya teknolojia ili kufanikisha maboresho hayo ya kisera. 

Ujumbe huo ulioongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara inayoshughulikia Utumishi wa Umma Bi. Catherine Musingwiire uliambatana na Mhe. Apolot Christine (MB) Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Utumishi wa Umma na Serikali za Mitaa; Mhe. Wokorach Peter (MB); Mhe. Baatom Koryang; Mhe. Nyangweso Denis (MB); Moses Bekabye mshauri wa Waziri wa Fedha; Byaruhanga Alex Mwanasheria Mwanadamizi wa Serikali; Opoti Jalmeo karani wa Kamati ya Bunge ya Utumishi wa Umma na Serikali za Mitaa na Afisa Ubalozi wa Uganda nchini Bi. Connie R. Nuwagaba. 

PSSSF hivi karibuni pia ilipokea ugeni kutoka Serikali ya Kenya, mashirikia ya Kimataifa ya IMF na World Bank kupitia ziara ambazo zimejikita kwenye kubadilishana uzoefu wa kitaalam na kujifunza masuala mbalimbali ya hifadhi ya jamii.

Mkurugenzi Mkuu PSSSF, CPA. Hosea Kashimba (kushoto) akiongozana na Katibu Mmuu Wizara ya Utumishi wa Umma nchini Uganda, Bi. Catherine Bitarakwate Musingwiire wakati yeye na ujumbe wake wakiwasili kwenye jengo la Golden Jubilee Tower jijini Dar es Salaam kwenye ziara ya kujifunza shughuli za PSSSF Mei 25, 2023.
Mkurugenzi wa Uendeshaji PSSSF, Bw. Mbarouk Magawa akitoa wasilisho lake kuhusu muundo na shughuli za PSSSF 
Mkurugenzi wa Uendeshaji PSSSF, Bw. Mbarouk Magawa akitoa wasilisho lake kuhusu muundo na shughuli za PSSSF
CPA, Hosea Kashimba.
Katibu Mkuu Wizara inayoshughulikia Utumishi wa Umma nchini Uganda, Bi. Catherine Musingwiire (kulia) akiongozana na Mkurugenzi wa Uendeshaji PSSSF, Bw. Mbarouk Magawa.

No comments