Header Ads

test

KAMPUNI YA SWISSPORT YAGAWA GAWIO BILION 1.5 KWA WANAHISA WAKE

Na.Khadija Seif,Michuziblog


KAMPUNI ya Swissport inatarajia kutoa gawio bilioni 1.5 kwa wanachama wake baada ya kupata faida kwa mwaka 2022.

Akizungumza na Wanahabari Leo Mei 25,2023 Mkurugenzi wa Kampuni ya Swissport Mrisho Yassin wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa hisa wa kampuni hiyo,mkutano huo wa 38 ambao ulikuwa na Agenda ya kupitisha mahesabu ya mwaka 2022 pamoja na kuzungumzia gawio la hisa kwa wanachama wake.

Yassin amesema mwaka 2022 ulikuwa mwaka mzuri wa kampuni baada ya miaka miwili iliyopita kupata mtikisiko wa kampuni kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Uviko 19.


"Tunafurahi matokeo ya fedha kiutendaji ndani ya kampuni yetu ilikuwa nzuri,baada ya kampuni kupata faida kabla ya kodi tumepata bilioni zaidi 3 mwaka 2022 tofauti na mwaka 2021 ambapo tulipata Bilion 2. huku baada ya kodi tumepata bilioni biliioni 2.5 kwa mwaka 2022 huku mwaka 2021 baada ya kodi tulipata 2.1".

Hata hivyo,Yassin amechanganua magawanyo wa Hisa kwa wanachama wake ambapo amesema kila shea moja kampuni italipa shilingi 41.8 ambayo jumla yake inafikia bilioni 1.5.

Yassini amesema kwa sasa wamejipanga kuwekeza zaidi kwenye teknolojia huku wanatazamia kutoa ajira zaidi kwa watanzania.

"Tunatambua mchango wa Rais wetu(Samia Suluhu Hassani) kupitia Filamu ya Royal Tour imefungua milango ya utalii hivyo sisi watumiaji wa sekta ya Anga tunatazimia kuwa na fursa kubwa ya uwekezaji hapa nchini"Amesema.

Kwa Upande wa Mwanahisa wa kampuni hiyo Emiliana Busara ameipongeza kampuni ya Swisport kutoa hisa kwa wanahisa huku akisema Gawio hilo linakwenda kuwabadilisha maisha yao .

"Kwa zaidi ya miaka 10 nimekuwa nikiweka hisa katika kampuni hii na ukiwekeza Swisport kuna faida mbalimbali ikiwemo kupata gawio ,imeambatana na sekta ya utalii na ni sekta inakuwa kwa kasi hivyo kadri ndege inavyoleta watalii nchini pato la taifa linaongeza zaidi na kampuni ya Swisport inapanuka pia.

Nae Mdau wa kampuni ya Swisport Mnaka Winani ameongeza kuwa sasa

Ongezeko la thamani 2022 ilikuwa hisa moja ilikua 100 na kwa sasa imepanda hadi hisa 1500 hivyo kampuni imerudi kwa kishindo na watu wameongeza zaidi kutokana na Uwelewa wa kila mtanzania kumiliki hisa yake.
Mwekezaji na mwanahisa Mnaka Winani akizungumza na Wanahabari Leo Mei 25,2023 na kueleza namna janga la uviko 19 lilivoiathiri kampuni hiyo na kupelekea hisa kushuka thamani kufikia 1000 kwa hisa na kwa mwaka  2023 hisa kupanda hadi 1500 kwa kila hisa
Mkurugenzi wa Kampuni ya Swissport Mrisho Yassin akizungumza na Wanahabari Leo Mei 25,2023 Jijini Dar es salaam wakati wa Mkutano mkuu wa mwaka wa hisa wa kampuni hiyo ikiwa na Agenda ya  kupitisha mahesabu ya mwaka 2022 pamoja na kuzungumzia gawio la hisa kwa wanachama wake. 


No comments