UBALOZI WA ITALIA NCHINI TANZANIA WATARAJIA KUSHEREHEKEA SIKU YA KITAIFA DAR
Na.Khadija Seif,Michuziblog
BALOZI wa Italia nchini Tanzania azindua rasmi Mwezi wa Tamasha la Siku ya Kitaifa kwa nchi ya italia "Festa della Repubblica" huku nchini Tanzania itatambulika kama "Tusherekee Italia kwa kuenzi lugha ya Kiswahili na mahusiano mazuri baina ya nchi hizo mbili.
Akizungumza na Wanahabari Leo Mei 25,2023 Balozi wa Italia nchini Tanzania Marco Lambardi amesema kutokana na uhusiano mzuri uliopo baina ya nchi mbili italia pamoja na Tanzania kwa takribani miaka 100 imepelekea Sekta mbalimbali kupanuka ikiwemo sekta ya teknolojia, kilimo,utoaji mafunzo na sekta ya utalii.
"Nchi ya Tanzania imekuwa na uhusiano imara na mzuri na nchi ya italia kwa kipindi chote cha 62 tangu kuwepo kwa ubalozi wake hapa Tanzania takribani Waitalia 10,338 waliandikishwa mwezi Januari 2023 kupitia uwanja wa ndege huku idadi kubwa ya watalii kuongezeka visiwani Zanzibar. ''
Hata hivyo Lambardi amesema Siku hiyo ya Kitaifa itasherehekewa na shughuli mbalimbali hadi mwezi Juni .
"Siku hiyo ya Kitaifa ya italia itasherehekewa mapema juni 02,2023, Pop _up shop Juni 03,2023 katika makazi ya balozi Tamasha la Kalascima na bendi ya italia Juni 08,2023 Slipway Jijini Dar es salaam .
Pia amesema sherehe zingine n8 Maonyesho ya pili Perugio pamoja na Uzinduzi wa mchezo wa tumia Akili Juni 22,2023 katika makazi ya balozi wa italia.Balozi wa Italia nchini Tanzania Mh. Marco Lambardi akizungumza na wanahabari Leo Mei 25,2023 nyumbani kwake Oysterbay Jijini Dar es salaam na kutambulisha rasmi Tamasha la kuenzi Siku ya Kitaifa ya Italia ambayo itaambatana na shughuli mbalimbali za kiburudani kuanzia Juni 02,2023 hadi Juni 22,2023
Post a Comment