Header Ads

test

UPEPO WABADIRIKA WIZARA YA NISHATI MANENO YAMEISHA


 

Na Humphrey Shao, Michuzi Tv

Ikiwa ni siku muhimu kwa watanzania kutokea makao Makuu ya nchi ya Dodoma Tanzania, Wizara ya Nishati inayoongozwa na Waziri January Makamba imeweza kuwasilisha makadirio ya Bajeti ya mwaka 2023/2024 Upepo umebadirika kwa wabunge.

Kama ilivyokuwa aikutegemewa kabisa kwa mchangiajinwa kwanza kabisa Mbunge wa Muleba Kaskazini, Charles Mwijage Alianza kwa kusifia maonesho ya WikiYaNishati yanayoendelea katika viwanja vya Bunge na kusema kuwa ni ‘maonesho ya karne’

Mwijage amesifu namna ambavyo kupitia maonesho hayo ameweza kupata majibu yote kuhusu umeme katika jimbo lake.

Wabunge wengine waliochangia katika BajetiYaNishati, nao wamepongeza maonesho hayo hususan ubunifu na matumizi ya teknolojia katika kuonesha maendeleo ya miradi ya nishati nchini.

“January Makamba nikupongeze sana kwa maono yako makubwa ambayo umeyaonesha katika Wizara yako. Mheshimiwa, tendo la kutuwekea maonesho yale, yani umeonesha ubunifu mkubwa na huu wala haujawahi kutokea. Hongera sana Mheshiwa Waziri Makamba, hii inadhihirisha kwamba wewe ni kijana mwenye maono, unategemea kufika mbali zaidi Mwenyezi Mungu akikuwezesha na tunaomba akuwezeshe” ni maneno ya Mbunge wa Mchinga, Salma Kikwete.

Maneno ya pongezi yaliyotolewa na Mbunge Salma Kikwete, yanaakisi pongezi zilizotolewa na Wabunge walitoa michango ya mwanzo katika Bajeti ya Nishati ambapo kwa kiasi kikubwa wamepongeza dira ya bajeti ya bajeti hiyo, maono na utendaji wa watendaji wa Wizara hiyo wakiongozwa na Waziri January Makamba.

Nae mbunge wa Kwimba, Shanif Mansoor mara baada ya kusimama kuchangia katika Bajeti ya nishati.

Katika mchango wake, Mansoor alimpongeza sana Waziri January Makamba na watendaji wa Wizara hiyo kwa kazi kubwa wanayofanya kiasi cha kuondoa kelele nyingi zilizokuwepo katika Wizara hiyo.

“Inaonekana kazi nzuri, mwaka huu Mheshimiwa Waziri umekuja hapa hakuna kelele kwenye Wizara ya Nishati, nakumbuka mwaka jana ulipofika hapa (kulikuwa na kelele)” amesema Mansoor.

Kwa upande wake Waziri January Makamba wakati akisoma hotuba yake ya bajeti, alisema anatambua kuwa Wizara anayoongoza ina maneno mengi na amewashukuru Wabunge kwa kuendelea kuwashauri. Pia alisema Wabunge wamemvumilia katika kipindi chote, na sasa mambo yameanza kukaa sawa.

Moja kati ya mambo makubwa kwenye Bajeti hii ya Nishati ni utekelezaji wa mradi wa Kuchakata na Kusindika Gesi Asilia kuwa Kimiminika (LNG). Maandalizi ya utekelezaji wa mradi huo yataanza katika mwaka ujao wa fedha.

Wabunge, Salma Kikwete (Mchinga) Charles Mwijage (Muleba Kaskazini), Katani Katani (Tandahimba), Elibariki Kingu (Singida Magharibi) kwa nyakati tofauti wamempongeza Waziri January Makamba kama msaidizi wa Rais katika sekta ya Nishati kwa kufufua mazungumzo ya mradi huo na sasa ndoto ya Rais inakwenda kutimia.

Kwa miaka takriban 8, majadiliano juu mradi huo yalikwama, lakini sasa Wizara ya Nishati chini ya Waziri Janaury Makamba kwa maelekezo ya Rais Samia Suluhu imeweza kufufua majadiliano hayo.
Waziri wa Nishati January Makamba akisoma makadirio ya Bajeti ya ya Wizara yake Bungeni  leo.
Sehemu  ya Wabunge wakiwa ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma.



No comments