Hospitali ya rufaa Simiyu, yapokea vifaa tiba huduma za kibingwa

Vitanda vilivyoletwa na Bohari kuu ya dawa (MSD) Kanda ya Ziwa kwa ajili ya huduma za kibingwa kwa akina mama wajawazito (Standard Electrical ICU Beds) katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Simiyu.

Afisa Usafirishaji kutoka Bohari kuu ya Dawa (MSD) Kanda ya Ziwa Haruni Kikwanda akikabidhi vifaa tiba ambavyo ni vitanda 9 kwa ajili ya huduma za kibingwa kwa akina mama wajawazito na watoto katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Simiyu. (kushoto) Ni mratibu wa huduma za Tiba Hospitali hiyo Dkt.Seleman Athuman.
Na Derick Milton, Simiyu.
Hospitali ya rufaa mkoa wa Simiyu imeanza kupokea vifaa tiba mbalimbali kutoka Bohara kuu ya Dawa (MSD) Kanda ya ziwa, kwa ajili ya kuanza kutoa huduma za kibingwa kwa akina Mama wajawazito na watoto.
Hatua hiyo inatajwa kuwa itaondoa kabisa adha iliyokuwepo katika mkoa huo, ambapo akina mama wajawazito na watoto waliohitaji huduma hizo walilazimika kupelekwa katika hospitali ya kanda Bugando Mkoani Mwanza.
Mratibu wa huduma za Tiba katika Hospitali hiyo Dkt. Seleman Athumani wakati akipokea vitanda 9 kutoka MSD kwa ajili ya huduma za kibingwa kwa akina mama wajawazito, ameishukuru MSD kwa kuwahisha vifaa hivyo.
Dkt. Athumani amesema kuwa malengo ya Rais Samia Suruhu Hassan ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma za Afya kwenye maeneo yao, yanakwenda kukamilika katika Mkoa wa Simiyu.
“ Awali mama mjamzito akihitaji huduma za kibingwa ililazimika kukimbizwa Bugando, Kilometa zaidi ya 150, lakini kwa sasa MSD wameleta hivi vifaa na vingine tayari wameishaleta, ndoto ya Rais Samia sasa inakwenda kukamilika,”….
“ MSD wameleta vifaa hivi ambavyo ni vitanda tisa, vina thamani ya zaidi ya Milioni 23, na vimekuja kwa wakati, jengo la akina mama na wajawazito nalo lipo katika hatua ya mwisho kukamilika, ndani ya mwezi mmoja huduma hii itapatikana hapa Simiyu,” amesema Dkt. Athumani.
Mratibu huyo ameipongeza MSD kwa huduma ambayo wamekuwa wakitoa katika hospitali hiyo, ambapo ameeleza mbali na vifaa hivyo wamekuwa wakipokea dawa pamoja na mahitaji mengine kwa wakati kutoka MSD.

Kwa upande wake Mganga mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Athanas Ngambakubi amesema kuwa MSD kuleta vifaa hivyo, huduma za Mama na mtoto zikiwemo za kibingwa zinakwenda kuhimalika katika hospitali hiyo.
Amesema kuwa ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto ujenzi wake umefikia asilimia 95, ambapo mafundi wanaendelea na ukamilishaji wa baadhi ya maeneo huku akibainisha kuwa ndani ya mwezi mmoja jengo litaanza kufanya kazi.
“ Tunashukuru MSD kwa vifaa hivi ambavyo wameleta mapema, kilichobaki ni vifaa vyenyewe kufungwa, na ujenzi wa jengo upo katika hatua ya mwisho, tunategemea ndani ya mwezi mmoja tutaanza kutoka huduma katika jengo hili,” amesema Dkt. Athanas.

Magodoro kwa ajili ya vitanda hivyo.
Je, una Tangazo, Picha za Matukio, Taarifa au Habari ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi 0746057557 au 0765402289 au Email : simiyupresstz@gmail.com

Post a Comment