MHANDISI LUHEMEJA: MTANDAO WA VIJANA KUANDALIWA NCHI NZIMA
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri
Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhandisi Cyprian Luhemeja
amesema Ofisi hiyo inatarajia kuandaa mtandao wa vijana nchi nzima ambao
utaratibu masuala yanayo wahusu vijana.
Mtandao huo utakuwa na
Maafisa vijana wa Wilaya na Mikoa ambao watahusika katika kutoa taarifa
zinazohusu vijana zikiwemo fursa zinazotolewa na serikali, Taasisi na
mashirika.
Mhandisi Luhemeja amebainisha hayo Oktoba 11, 2023
Babati Mkoani Manyara katika kongamano la Maadhimisho ya wiki ya vijana
kitaifa.ambapo amesema amesema lengo la Serikali ni kuona vijana wana
mtandao mmoja ambao unarahisisha kuwafikia kwa wakati.
Amesema
Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan tayari ameweka mazingira wezeshi kwa
vijana ambayo yanampa fursa ya kujikwamua kiuchumi, hivyo wajitambue,
wajitume, wafanye kazi kwa weredi na ubunifu serikali itawaunga mkono.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhandisi Cyprian Luhemeja,akizungumza katika kongamano la Maadhimisho ya wiki ya vijana kitaifa Babati Mkoani Manyara.
Post a Comment