Header Ads

test

TPBRC YAMFUNGIA MWAKINYO MWAKA 1 NJE YA ULINGO

 

Na.Khadija Seif,Michuziblog. 

KAMISHENI ya Kusimamia Ngumi za Kulipwa nchini (TPBRC) imefungia bondia Hassan Mwakinyo mwaka mmoja kutojihusisha na mchezo wa Ngumi Ndani na nje ya nchi na kulipa faini ya milioni moja.

Kabla ya maamuzi hayo TPBRC ilitoa siku Saba Kwa bondia Hassan Mwakinyo na Promota wa Paf Promotion kuleta vielelezo sababu za kutopanda ulingoni katika Pambano hilo ambavyo waliviwasilisha.
Adhabu hiyo imekuja baada ya Mwakinyo kugomea kupanda ulingoni dhidi ya Raia Mnamibia Julius Indongo Katika Pambano liliandaliwa na Paf Promotion ambalo lililotakiwa kupigwa Septemba 29 mwaka huu Dar es Salaam.

Akizungumza na Wanahabari Leo Oktoba 10,2023 Jijini Dar Es Salaam Katibu Mkuu wa TPBRC George Silasi Lukindo,amesema kuwa adhabu hiyo sio kwa mwakinyo bali ni kwa mabondia wote waliyopo chini ya kamisheni.

Silasi amesema kuwa mabondia wanatakiwa kuheshimu na wasikiuke taratibu na sheria za mchezo huo kwani hakuna bondia aliye juu ya kamisheni hiyo.

"Kamisheni kupitia Kamati ya nidhamu ulipokea maelezo ya pande zote ya Mwakinyo na Promota wa Paf promotion Godson Karigo na imeona Mwakinyo ndio mwenye makosa yakutoheshimu mkataba imetoa adhabu hii ambao imeanza Leo Oktoba 10,2023 hadi Oktoba 10 mwaka 2024."

Katibu huyo amefafanua zaidi kuwa TPBRC imetoa haki ya bondia huyo kukata rufaa ndani ya siku Saba baada ya kupewa adhabu hiyo.

No comments