Header Ads

test

Prof.Ndalichako:Taratibu ya kusitisha maadhimisho ya miaka 30 ya CWT hayako sawa

 

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

Serikali imesema kuwa mambo yanayoendelea katika Chama cha Walimu Tanzania (CWT) hajui chochote kutokana na chama hicho hakijapeleka malalamiko yeyote.

Hayo ameyasema Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako siku moja baada ya chama hicho kutoa taarifa katika mitandao ya jamii kuhusiana na kustisha kufanyika kwa maadhimisho ya miaka 30 kutokana kutokuwepo kwa Mgeni Rasmi Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Prof.Ndalichako amesema Rais kutokuwepo sio ndio kufanya maadhimisho hayo kustisha na taratibu zilizotumika ya kustisha maadhimisho sio sahihi.

Amesema kuwa tarehe zilizokuwa zinapangwa zilikuwa zikiingiliana na majukumu mengine ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan hivyo walitakiwa kupanga tena na sio kupisha ujumbe katika mitandao ya Jamii.

"Serikali hatuna taarifa yeyote juu ya kinachoendea kwenye Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kuwa kuna migogoro hiyo migogoro ndio nasikia hapa lakini Serikali hatuna taarifa hizo.

Amesema maombi yao ya kutaka mgeni Rasmi yalikubaliwa lakini CWT kwa Mwezi wa 10 yalikubaliwa wakaomba kusogeza muda na kusogeza kutokana majukumu ya Rais yaliingiliana na majukumu mengine.

Aidha amesema Rais anathamini kazi ya CWT na Walimu kwa kazi zao na kuwa karibu katika kutatua changamoto zao.

Amesema kubadiika kwa tarehe kwa Rais na majukumu yake inakuwa changamoto ambapo sio nia yake ya kutotaka kuwa mgeni rasmi.

Amesema kuwa walimu wote nchini na CWT itaendelea kushirikiana hatua kwa hatua pamoja na kuendelea kuboresha mazingira walimu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Chama cha Walimu Tanzania  (CWT) kusitisha maadhimisho ya miaka 30 ya Chama hicho kwa kutoa taarifa Mtandaoni jijini Dar es Salaam.

No comments