Header Ads

test

WAZIRI BASHE MGEMI RASMI KUTANO WA CROSAT

Farida Mangube Morogoro 

Waziri wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mkutano mkuu wa Chama Cha Taaluma ya Sayansi Kilimo Mazao Tanzania (CROSAT) kitakachofanyika Jijini Dodoma Disemba 19- 20 mwaka huu.

Mkutano huo  unalenga Kujadili masuala mbalimbali ya Kilimo Mazao hasa matumizi sahihi ya viuatilifu ambao utahudhuliwa na zaidi ya wanachama mia mbili.

Akizungunza na waandishi wa Habari  Katibu  mkuu wa Chama hicho Patrick Ngwediagi amesema hivi sasa kumekua na changamoto ya matumizi holela ya viuatilifu bila ya kufuata ushauri wa Watalam  jambo ambalo ni hatari kwa afya ya walaji.

Ngwediagi amesema licha ya serikali kuwekeza fedha nyingi kwenye miradi ya Kilimo bado wakulima wanahitaji elimu ya Kilimo bora chenye tija Ili kujikomboa kiuchumi.

Katika mkutano huo pia itajadiliwa ajenda ya kupitisha katiba ya chama hicho pamoja semina ya  kitaalum Kwa Wataalamu wa Kilimo na wadau wa sekta hiyo Kwa ujumla Disemba 19  .

Kwa upande wake Dkt.Yasinta Nzogale Katibu Msaidizi wa Chama CROSAT amesema pia wanalenga kusaidia wanawake kupitia Kilimo kwa kuwapatia elimu na mbinu bora za Kilimo



 

No comments