RAIS MWINYI: SMZ KUJENGA KIWANJA KIPYA CHA MPIRA - AFCON2027
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameendelea na ziara ya kikazi nchini China ambapo leo amekutana na kampuni mbalimbali zinazolenga kuwekeza Zanzibar. Katika mwendelezo wa ziara hiyo Rais Dk. Mwinyi pia, amekutana na uongozi wa kampuni maarufu na yenye uzoefu wa miaka mingi, China Railway Construction Engineering Group (CRJE), yenye makao makuu Beijing, China katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Westin, Shanghai, China.
Katika mkutano huo, Rais Dk. Mwinyi ameeleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina mpango wa kujenga Mji wa Kiserikali ambapo Serikali na taasisi zake zitawekwa sehemu moja ili kuboresha ufanisi na utendaji serikalini pamoja na kurahisisha huduma kwa wananchi.
Rais Dk. Mwinyi ameongeza kuwa Serikali pia ina mpango wa kujenga kiwanja cha mpira wa miguu cha kimataifa kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2027.
Mkutano huo umekutanisha Benki na taasisi za fedha, wakiwemo wenyeji CRJE, China Dasheng Bank of Tanzania, Jiangsu Financial Leasing Co. Ltd, Huaxia Bank, Citic Bank, na Bank of Shanghai, ambao wamekuja kujadili fursa za uwekezaji na ushirikiano wa fedha katika miradi mbalimbali ya maendeleo Zanzibar.
Aidha, Rais Dk. Mwinyi amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ipo tayari kushirikiana na wadau wote wa fedha na wawekezaji ili kufanikisha miradi hiyo.
Post a Comment