Header Ads

test

Dkt. Abbas: Ushirikiano wa Wadau Muhimu Kukabiliana na Tabianchi

 

 

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbas, amewataka wadau wa maendeleo wakiwemo WWF kuendelea kushirikiana na Serikali katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na ulinzi wa misitu nchini.

Dkt. Abbas alitoa rai hiyo jijini Dar es Salaam, Septemba 11, 2025, wakati wa hafla ya uzinduzi wa vifaa vya usimamizi wa misitu na huduma za ugani vilivyotolewa kupitia mradi wa mbinu za pamoja za upatikanaji wa nishati, unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya kupitia WWF.

“Serikali imefanya jitihada kubwa kulinda rasilimali za misitu kwa kutoa elimu na kampeni za uhifadhi, lakini changamoto za tabianchi ni kubwa, zinahitaji mshirikiano wa karibu na wadau,” alisema Dkt. Abbas.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo, alisema karibu asilimia 75 ya kaya bado zinategemea nishati ya mimea, hali inayoongeza shinikizo kwenye misitu. Alisisitiza kuwa Serikali inaimarisha kampeni ya matumizi ya nishati safi ya kupikia, kampeni inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Naye, Mkurugenzi wa WWF, Dkt. Amani Ngusaru, alisema shirika hilo limekuwa likishirikiana na Serikali kwa zaidi ya miaka 30 katika kusaidia uhifadhi wa misitu na litaendelea kuwajengea uwezo wadau kuhakikisha hifadhi zinabaki salama.

Mradi huo unaogharimu zaidi ya shilingi bilioni moja umewezesha ununuzi wa magari, pikipiki, boti ya mwendokasi, vifaa vya TEHAMA, jenereta pamoja na mifumo ya kisasa ya ufuatiliaji, hatua inayotarajiwa kuongeza ufanisi wa taasisi za Serikali katika uhifadhi wa misitu.




































No comments