Header Ads

test

OCPD yapongeza Ushirikiano na Ofisi ya Mashitaka katika zoezi la Urekebu wa Sheria

 

 

 Na: Calvin Gwabara – Dodoma.

Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria (OCPD) imekabidhi Juzuu za toleo la Urekebu wa Sheria la mwaka 2023 kwa Ofisi ya Taifa ya Mashitaka na kupongeza mchango mkubwa uliotolewa na Ofisi hiyo kupitia watumishi wake kwenye utekelezaji wa zoezi la Urekebu. 

Mkurugenzi wa Mashitaka Bw. Sylvester Mwakitalu (Kulia) akipokea Juzuu kutoka kwa  Kaimu Mkurugenzi wa Divisheni ya Urekebu,Tafiti na Mafunzo Bi. Rehema Katuga.Akikabidhi Juzuu hizo kwa Mkurugenzi wa Mashitaka Bw. Sylvester Mwakitalu, Kaimu Mkurugenzi wa Divisheni ya Urekebu,Tafiti na Mafunzo kwa naiaba ya  Mwandishi Mkuu wa Sheria Bi. Rehema Katuga amepongeza ushirikiano Mkubwa ambao Ofisi ya Mashitaka imeutoa wakati wa mchakato mzima wa utekelezaji wa zaoezi hilo na kuchangia kukamilika kwa zoezi hilo la kihistoria.

“Wakati tunaanza zoezi hili Ofisi yetu ilikuwa na changamoto kubwa ya uhaba wa watumishi hasa Mawakili wa kufanya kazi hii lakini tulikuwa tukibisha hodi kwenye Ofisi yako kuomba Mawakili kuja kushirikiana nasi katika kutekeleza zoezi hili, na hakika walitusaidia sana hadi tumekamilisha” alieleza Bi Katuga.

Aliongeza“ Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria kwa kutambua mchango wenu imeona ni muhimu na Ofisi yako pia ipate nakala hizi ingawa tunatambua kuwa tumeleta chache kutokana na gharama lakini ziwasaidie kwa kuanzia na kuwa kama kumbukumbu kwenu, lakini mnaweza kupata nakala laini zote kupitia mfumo wa OAG MIS library” Alieleza Bi. Katuga.

Kaimu Mkurugenzi huyo wa Divisheni ya Urekebu,Tafiti na Mafunzo ameongeza kuwa pamoja na nakala hizo tano pia wameipatia Ofisi hiyo tuzo maalumu kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa lengo la kutambua mchango wa Ofisi ya Taifa ya Mashitaka katika zoezi hilo la Urekebu wa Sheria.

Akizungumza kwa niaba ya watumishi wa Ofisi yake Mkurugenzi wa Mashitaka Bwana Sylvester Mwakitalu amepongeza kazi kubwa iliyofanywa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupitia Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria (OCPD) na kushukuru  kwa kuwapatia nakala hizo za kuanzia kwaajili ya Ofisi yake maana wangeenda kununua dukani ingekuwa gharama kubwa.

“Ofisi yetu tunatumia Sheria hizi kila siku maana tunatoa huduma za mashitaka kwenye mahakama zote nchini hasa hasa mahakama za Wilaya na za Hakimu Mkazi ndiko tunaenda huko kila siku,lakini pia mahakama kuu na mahakama ya Rufaa, kwahiyo hizi Sheria ni nyenzo muhimu sana kwetu” Alieleza Bwana Mwakitalu.

Aliongeza” Nakala hizi tulizozipata tutazisambaza kwa Mawakili wetu kwanza, alafu sisi tutaendela kusubiria kupata zingine kwa utaratibu maalumu lakini pia kwa kutumia zle ambazo zinazopatikana kwenye mfumo kwa nakala tepe”.

Toleo la Urekebu wa Sheria la Mwaka 2023 lilizinduliwa na kwa mujibu wa Sheria na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan mwezi wan ne mwaka huu na kutangaza kuanza kutumika tarehe 1/07/2025 na hivyo kufuta Toleo la sheria la mwaka mwaka 2002.

Kaimu Mkurugenzi wa Divisheni ya Urekebu,Tafiti na mafunzo kutoka OCPD  Sheria Bi. Rehema Katuga akikabidhi tuzo maalumu kwa Mkurugenzi wa Mashitaka Bwana Sylvester Mwakitalu  kutambua mchango wa ofisi hiyo katika utekelezaji zoezi la Urekebu wa sheria la mwaka 2023.

Mkurugenzi wa Mashitaka Bwana Sylvester Mwakitalu  akitoaa neno la shukrani kwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupitia Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria.

Mkurugenzi wa Mashitaka Bwana Sylvester Mwakitalu  pamoja na maafisa wengine wa ofisi yake wakibadilishana mawazo wakati wa hafla hiyo ofisini kwake.
Mkurugenzi wa Mashitaka Bwana Sylvester Mwakitalu  akifurahia moja ya juzuu alizokabidhiwa.
Picha ya pamoja ya Maafisa wa Ofisi ya Taifa ya Mashitaka na Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria mara baada ya hafla hiyo.
Kaimu Mkurugenzi wa Divisheni ya Urekebu,Tafiti na Mafunzo Bi. Rehema Katuga akionesha moja ya juzuu hizo za toleo la Urekebu wa sheria za Mwaka 2023.

No comments