Header Ads

test

MARY CHATANDA AMUOMBEA KURA DK.SAMIA MKURANGA, AMPIGIA DEBE ULEGA MKURANGA

Na Mwandishi Wetu,Mkurunga 


MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania(UWT) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mary Chatanda amesema Chama hicho  kimewateua wagombea wanaokubalika kuelekea Uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29 mwaka huu.

Hivyo amesema jukumu kubwa la wananchi ni kuhakikisha wanawachagua wagombea wa Chama hicho kuanzia nafasi ya Urais ,wabunge na madiwani kwa  kuwapa kura nyingi za ndio ifikapo otoba 29,mwaka huu

Chatanda ameyasema hayo wakati wa  uzinduzi wa kampeni Jimbo la Mkurunga  ambapo yeye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi ambapo amesema  katika kipindi cha  uongozi wa Dkt .Samia  Suluhu Hassan ameweza kutekeleza miradi mingi ya maendeleo.

Kuhusu kampeni Chatanda amesema mkoa wa Pwani kupitia wabunge waliokuwepo katika Mkoa huo wamefanya kazi nzuri na wengi wao wameweza kuteuliwa kuwa mawaziri kutokana na uchapakazi wao .

Aidha amewaomba wananchi kumpa kura nyinyi mgombea Urais wa CCM Rais Dk.Samia kwani wakimpa miaka mingine mitano atakwenda kufungua fursa za uwekezaji na hivyo kuongeza wigo wa ajira kwa vijana wa Mkuranga.

Ametumia nafasi hiyo pia kuzungumzia taarifa zinazoenea kwenye mitandao ya kijamii ambapo amewaomba wananchi  kuwaachana nazo na kuhakikisha wanamchagua Dkt Samia kwa kishindo ili vituo vya afya,zahati ,na maeneo mengine yanaendelea kuboreshwa.

Kuhusu Ulega amewaomba wananchi kuhakikisha wanamchagua mgombea ubunge huyo. “Ndugu zangu niwaombe tukamchague Ulega na tayari  mlishafanya kazi kubwa kupitia kura za maoni na Chama kimemteua Ulega kugombea Jimbo hili, hivyo hakikisheni  mnakuwa naye  kwenye kampeni zake kote atakakopita."amesema Chatanda 

Awali Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji UWT na Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Pwani Mariam Ulega amewashukuru wananchi wa Mkoa wa Pwani kwa kumchagua yeye kuwa Mbunge Viti maalum .

Pia amemshukuru Mwenyekiti  Chatanda  kwa kumteua kwenda kuwaombea kura  wagombea wa CCM huku akitoa rai kwa wananchi kuhakikisha wanampigia kura  Dkt.Samia ,Mgombea ubunge Abdallah Ulega pamoja na wagombea udiwani.

Kwaupande wake Mbunge wa Jimbo la Kondoa mjini Mariam Ditopile akizungumza katika uzinduzi huo amewataka wananchi wa Mkuranga kupiga kura nyingi kwa Dkt.Samia Suluhu Hassan na Abdallah Ulega .










No comments