Header Ads

test

FEMATA YAWASISITIZA WACHIMBAJI KUSHIRIKI MAONESHO YA MADINI YA KIMATAIFA.



Na Joel Maduka Shinyanga.

Rais wa Shirikisho la wachimbaji wadogo wa madini Nchini(FEMATA),John Bina amewataka wachimbaji wadogo kushiriki kwenye maonesho ya Madini ya Kimataifa ambayo yanatarajia kuanza kesho tar 22 Sept 2023 Mjini Geita.

Bina amesema hayo mapema leo wakati akiwa kwenye ziara yake ya siku moja ya kikazi Mkoani Shinyanga ambayo ilikuwa imelenga kuzungumza na wachimbaji na kuwaeleza juu ya leseni ambazo hazijakizi vigezo vya uchimbaji.

Amesema ni vyema kwa wachimbaji wadogo wakajitokeza kwa wingi kushiriki kwenye maonesho ya madini ya Kimataifa yanayoanza kesho kwenye viwanja vya Bomba mbili Mjini Geita.

“Jambo la msingi pia ambalo nataka kuwakumbusha wachimbaji ni taarifa ya kufutwa kwa leseni ambazo hazijakizi vigezo niwaombe wachimbaji zimeongezwa siku 15 ambazo zimetolewa na Waziri wa Madini siku hizi zinaisha tar 30 mwezi huu niwasihi sana kwenda kwenye ofisi ya madini za mikoa kwaajili ya kuweka sawa taarifa zenu”John Bina Rais wa FEMATA.

“Lakini pia tar 23 mwezi huu sisi Shirikisho tutatoa tuzo kwa Mhe,Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati,Doto Biteko ambaye kwa kiasi kikubwa alikuwa ni Waziri kwenye Wizara yetu ya madini tunataka kumshukuru kwa namna alivyoweza kutusimamia nitoe Wito wachimbaji kuwepo siku hiyo ya Tar 23 mjini Geita kwaajili ya kuja kusherekea na kumpongeza Naibu Waziri Mkuu”John Bina Rais wa FEMATA.

No comments