Header Ads

test

PROF. NDALICHAKO AKIPONGEZA KIWANDA CHA MBOLEA CHA ITRACOM KWA UTEKELEZAJI SHERIA ZA KAZI



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (wa pili kutoka kushoto) akimsikiliza Msimamizi Mitambo wa kiwanda cha uzalishaji Mbolea cha Introcom Fertilizer Limited Eng. Peter Nchuma (wa pili kulia) akielezea hatua za uzalishaji wa mbolea katika kiwanda hicho. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri.

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amekipongeza kiwanda cha mbolea cha ITRACOM Fertilizer Limited kwa kuzingatia sheria za kazi ikiwemo kuwapa mikataba wafanyakazi, Usalama na afya mahali pa kazi na kuwasilisha michango ya wafanyakazi kwenye mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa wakati.

Prof. Ndalichako ameyasema hayo Septemba 18, 2023 alipofanya ziara ya kutembelea kiwanda hicho kilichopo jijini Dodoma kwa lengo la kukagua utekelezaji wa Sheria za kazi, ambapo amewataka wawekaji nchini kuiga mfano kwa ITRACOM.

Waziri Ndalichako amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuweka mazingira wezeshi ya wawekezaji nchini , uwekezaji wa kiwanda hicho cha mbolea umezalisha ajira za awali 1,198 na kitakapokamilika ajira moja za kwa moja 3500 zitazalishwa na ambazo sio za moja kwa moja zitazalishwa ajira 8000.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri ameahidi kuendelea kuimarisha mazingira wezeshi kwa wawekezaji ili uwekezaji wa kiwanda hicho uweze kukamilika kwa wakati na kuwa na tija kwa wananchi.

Mkurugenzi wa Uratibu wa Ndani wa Kiwanda hicho, Kimaramuziro Nkurikiye ameshukuru serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia kwa kuendelea kutoa ushirikiano kwenye ujenzi wa kiwanda hicho na kutatua changamoto zilizokuwa zinawakabili ikiwemo maji, Umeme, na Barabara.

Aidha, Katika ziara hiyo Waziri Ndalichako aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri pamoja na viongozi na watendaji yake na Taasisi zilizochini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akizungumza viongozi na wafanyakazi wa kiwanda cha kuzalisha mbolea Itracom Fertilizer mara baada ya kukagua utekelezaji wa sheria za kazi katika kiwanda hicho tarehe 18 Septemba, 2023 jijini Dodoma. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe. Jabir Shekimweri. Kulia ni Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Kiwanda cha Itracom, Kimramzilo Nkurikiye.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri akieleza jambo wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu) Prof. Joyce Ndalichako (hayupo pichani) wakati wa ziara yake ya kutembelea maeneo ya kazi katika Mkoani Dodoma akiambatana na Viongozi wa Taasisi zilizochini ya Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na watendaji wengine katika kiwanda cha uzalishaji mbolea Itracom Fertilizer Limited.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akisikiliza maelezo kuhusu aina ya mbolea zinazozalishwa kiwandani hapo kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Biashara na Masoko wa Kiwanda cha uzalishaji mbolea cha Intracom Fertilizer Limited Dkt. Keneth Masuke (kushoto) wakati wa ziara hiyo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (wa pili kutoka kushoto) akimsikiliza Msimamizi Mitambo wa kiwanda cha uzalishaji Mbolea cha Introcom Fertilizer Limited Eng. Peter Nchuma (wa pili kulia) akielezea hatua za uzalishaji wa mbolea katika kiwanda hicho. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (katikati) akiangalia Mchanga aina ya Phosphete unaotumika kutoa sumu kwenye udongo kabla ya kupanda mazao. Wa tatu kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha kuzalisha mbolea cha Itracom Fertilizer Limited wakati wa ziara hiyo.

Mkurugenzi wa Uratibu wa Ndani wa kiwanda cha uzalishaji mbolea Itracom Fertilizer Limited, Kimaramuziro Nkurikiye akitoa taarifa kuhusu kiwanda hicho wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako (kushoto) katika kiwanda hicho Mkoani Dodoma.

Kamishna wa Kazi, Suzan Mkangwa (kushoto) akitoa taarifa ya ukaguzi wa utekelezaji wa sheria za kazi katika kiwanda cha uzalishaji mbolea Itracom Fertilizer Limited wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako katika kiwanda hicho Mkoani Dodoma.

PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)

No comments