Header Ads

test

MSIGWA AZINDUA 3 KUBWA ZA BASATA ASISITIZA MAADILI KWA WASANII

 

WIZARA Ya Sanaa Utamaduni na Michezo imesema ina mipango ya kuunda mkakati wa ukuzaji wa sanaa, kwa kuanisha maeneo yenye mafanikio na kuyaangazia, pamoja na kuangalia njia za kuboresha maeneo yenye changamoto.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Gerson Msigwa wakati akizindua Tatu Kubwa za Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) amesema mkakati huo utajikita katika kukuza shughuli zinazohusiana na sanaa, kuongeza ufikiaji wa sanaa kwa watu wa ndani na nje ya nchi.

Msigwa ameeleza kuwa kwa kuzingatia tasnia inayoongoza kwa ukuaji katika uchumi wa mwaka jana, angependa kuona tasnia hiyo ikidumisha kasi yake ya ukuaji.

“Mafanikio hayo yanaweza kupatikana kwa juhudi za pamoja za viongozi wa serikali, taasisi na wadau."

Katika kubwa tatu, kulikuwa na uzinduzi wa muongozo wa uzingatiaji wa maadili katika kazi ya sanaa ambapo Msigwa amesema miongozo ya maadili inalenga kuwawezesha wasanii kufanya kazi kwa raha na kukumbatia tamaduni za Kitanzania badala ya tamaduni za kigeni.

Katibu Mtendaji wa Basata Dkt. Kedmon Mapana amesema miongozo hiyo inalenga kuwawezesha wasanii na wadau wa sanaa kushiriki moja kwa moja katika kulinda maadili wakati wa kuandaa kazi zao za sanaa.

Pili, inalenga kutatua changamoto za ukiukwaji wa maadili unaotokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia katika sekta ya sanaa.

Lengo lingine amesema ni kuilinda jamii dhidi ya vitendo vinavyokwenda kinyume na kanuni za maadili, hasa kuwalinda watoto dhidi ya maudhui yasiyofaa yanayoweza kukwamisha maendeleo yao, kuhakikisha usalama wa taifa, kukuza amani, na kukuza mshikamano ndani ya jamii.

Pia ametoa rai kwa wasanii kutengeneza kazi zenye Maadili kwani wao wamebeba maisha ya watu hivyo kubomoa au kujenga itatokana na sanaa huku akimtoa mfano Mwamuziki kutoka Wasafi Nasib Abdul maarufu kama "Diamond platinum " kuwa na wafuasi wengi mtandao wa kijamii ambao wanamfatilia hivyo mtandao huo ukitumika vizuri  unaweza kuleta tija kwa jamii.

Mbali na muongozo, kulikuwa na uzinduzi wa Bodi ya Barza la Sanaa la Taifa na Kamati ya Kitaifa ya Tuzo za Muziki (TMA).

Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa Utamaduni na Michezo Gerson Msigwa akizungumza na Wanahabari pamoja na Wadau wa Kazi za Sanaa Jijini Dar es Salaam wakati wa Kuzindua tatu kubwa za Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ikiwemo Kamati ya Tuzo za Muziki nchini (TMA),Muongozo wa uzingatiaji wa maadili katika kazi ya sanaa pamoja na Kutambulisha Bodi ya Wajumbe wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA)

 

Picha ya Pamoja Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaaa na Michezo  Gerson Msigwa akiwa na Wajumbe wa Bodi ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) wakati akizindua  Mwongozo wa Maadili katika Sanaa, Kamati ya Kitaifa ya Tuzo za Muziki na Bodi ya Baraza la Sanaa la Taifa.

No comments