ORYX GAS YAWAKUMBUKA WATUMISHI, WAJASIRIAMALI WILAYANI MAFIA, YAGAWA BURE MITUNGI YA GESI 200
Mwandishi Wetu, Mafia
KAMPUNI ya Oryx Gas Tanzania kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Mafia mkoani Pwani Zefania Sumaye wamekabidhi mitungi 200 yenye ujazo wa kilo 10 pamoja na majiko bure kwa makundi mbalimbali ya wananchi wilayani humo.
Miongoni mwa makundi ya wananchi waliopewa mitungi hiyo ya gesi ni walimu, wahudumu wa afya,askari polisi na wanawake wajasiriamali huku kampuni hiyo ikisisitiza jamii kutunza mazingira kwa kutumia nishati safi ya kupikia na kuachana na matumizi ya kuni na mkaa.
Akizungumza wakati wa ugawaji wa mitungi hiyo kwa wananchi wa Mafia, Mkuu wa Idara ya Mauzo Oryx Gas Shaban Fundi amesisitiza kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Mafia wameamua kuungana kuunga mkono juhudi za serikali katika utunzaji wa mazingira ya kisiwa hicho.
Pia amesema mbali na kutunza mazingira matumizi ya nishati safi yanalenga kulinda afya za akina mama pamoja na usalama wa wototo kwa kuwahakikishia upatikanaji wa nishati safi ya kupikia kwa wakazi wa Mafia.
"Kampuni yetu kupitia wakala wetu mkuu Tash Oil, inawahakikishia wananchi upatikanaji wa nishati safi ya kupikia bila matatizo na hii inalenga kutoa suluhisho la muda mrefu la upatikanaji finyu wa bidhaa hiyo kisiwani hapo, " amesema Fundi
Amesisitiza Oryx Gas pia imedhamiria kutoa suluhisho kwenye taasisi mbalimbali kama magereza na shule ili ziweze kuacha kutumia kuni na mkaa na kujikita katika matumizi ya nishati safi ya kupikia ambayo ni gesi ya Oryx.
Ameongeza kwa upande wa viwanda vya kuchemsha dagaa katika kisiwa cha Mafia ambao ndio watumiaji wakubwa wa kuni katika shughuli hiyo, Oryx itawapatia majiko yanayotumia gas ili kuepuka athari za kiuchumi, afya na mazingira.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mafia Zefania Sumaye ameishukuru Oryx Gas kwa kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutunza mazingira na uwezeshaji wananchi.
Amesisitiza wananchi kuacha kuni na kutumia nishati safi ya kupikia huku akiiomba kampuni ya Oryx kupeleka huduma hiyo kwenye viwanda vya kuchemsha dagaa ambavyo ni watumiaji wakubwa wa kuni kisiwani humo.Mkuu wa Wilaya ya Mafia mkoani Pwani Zefania Sumaye(katikati)akiwa na Meneja Mauzo wa Oryx Gas Shaban Fundi(wa pili kushoto) wakikabidhi mtungi wa gesi wa kilo 10 kwa baadhi ya wanawake wajasiriamali wilayani hapa.Oryx Gas kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Mafia Sumaye wamegawa bure bure mitungi ya Oryx pamoja na majiko yake 200 kwa wananchi wa makundi mbalimbali wa wananchi wa wilaya hiyo wakiwemo walimu, watumishi wa kada ya afya,vyombo vya ulinzi na wajasiriamali
Post a Comment